Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu wa Timor Leste Wamepiga Kura katika Uchaguzi wa Bunge

Watu wa Timor Leste Wamepiga Kura katika Uchaguzi wa Bunge

Raia wa Timor Leste takribani 600,000 mwishoni mwa wiki wamejitokeza kuwasilisha sauti zao kwa njia ya kura kwenye uchaguzi mkuu wa bunge mwaka 2012. Kama kawaida vituo vya upigaji kura vilifunguliwa mapema asubuhi na kulishuhudiwa misruiru mirefu ya watu wenye hamasa na hamu ya kutekeleza haki yao ya kuchagua viongozi wanaowataka.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameipongeza serikali ya Timor Leste na hususan sekretariati ya kiufundi ya uchaguzo na tume ya taifa ya uchaguzi kwa kuandaa na kusimamia uchaguzi huo. Pia amelisifu jeshi la polisi la nchi hiyo kwa kuhakikisha mazingira ya amani ya usalama wakati wote wa uchaguzi.

Kwa mujibu wa duru za habari nchini humo matokeo ya awali ya uchaguzi yaliyoanza kutoka Jumapili jioni yanaashiria kwamba chama cha waziri mkuu Xanana Gusmao kinaelekea kushinda huku chama kikuu cha upinzani Fretilin kikishika nafasi ya pili.