Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yapeleka misaada ya dharura kwa wahamiaji wanaorejea nyumbani kaskazini mwa Chad.

IOM yapeleka misaada ya dharura kwa wahamiaji wanaorejea nyumbani kaskazini mwa Chad.

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM na chama cha mwezi mwekundu nchini Chad wanapeleka misaada ya dharura kwenye mji ulio kaskazini mwa nchi wa FayaLargeau ambapo tayari wahamiaji 300 wamewasili kutoka Libya siku mbili zilizopita.

Wahamiaji hao 300 ni kati ya kundi la watu 1000 waliorejeshwa nchini Chad na utawala wa Libya kwa kuishi nchini Libya bila ya vibali kamili. Kulingana na wahamiaji hao baadhi yao walikuwa wamezuiliwa vituoni huku wengine wakiamua kurudi nyumbani kufuatia ghasia zinazoshuhudiwa kusini mwa Libya. Jumbe Omari Jumbe ni afisa wa IOM

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)