Baraza la Haki za Binadam lalaani ukiukaji mkubwa wa haki za binadam Syria

6 Julai 2012

Baraza la Haki za Binadam la Umoja wa Mataifa, leo limelaani vikali ukiukaji mkubwa wa haki za binadam nchini Syria, pamoja na mauaji na mashtaka yanayoendelezwa dhidi ya waandamanaji, wanaharakati wa haki za binadam na waandishi wa habari.

Katika azimio lililoungwa mkono na nchi 41 wanachama, Baraza hilo limesisitiza umuhimu wa kuwafikisha wale wanaopanga na kueneza ghasia dhidi ya watu wa Syria. Nchi tatu, zikiwemo Cuba, Uchina na Urusi, zimepinga azimio hilo. India, Ufilipino na Uganda zimejiondoa na kutounga mkono upande wowote.

Baraza hilo limefanya uamuzi wa kuwasilisha ripoti zake zote na hoja za ziada kwa idara husika za Umoja wa Mataifa na kwa Katibu Mkuu ili hatua zinazofaa zichukuliwe.

Akizungumza kwenye Baraza hilo, mwakilishi wa Marekani, Eileen Chamberlain Donhoe alikuwa na haya ya kusema

(CLIP YA CHAMBERLAIN)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud