Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tatizo la Kukosa Makazi Haiti sasa linakaribia kufikia Ukomo

Tatizo la Kukosa Makazi Haiti sasa linakaribia kufikia Ukomo

Juhudi zinaendelea kuchukuliwa kukamilisha ujenzi wa nyumba zilizoharibiwa kutokana na tetemeko lililoikumba Haiti ambalo lilivuruga ustawi wa eneo hilo na kuacha mamia ya watu bila makazi.

Katika jitihada zake za mwisho mwisho shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM limeendesha operesheni ya kuzijenga upya nyumba zilizoharibiwa katika mji mkuu wa utamaduni Jacmel.

Kukamilika kwa mpango huo kutafanya kambi mbili zilizoanzishwa kwenye eneo hilo baada ya tetemeko la mwaka 2010 kufungwa. Kambi hizo zinachukua kiasi cha familia 36.

Wakati watakapoondolewa kwenye kambi hizo, familia hizo zinapatiwa mafungu ya fedha kwa ajili ya kugharimia pango za nyumba kwa kipindi cha mwaka mmoja na wakati huo huo wakipatiwa fedha za kujikimu kimaisha.