Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa Rio+20 Ulikuwa na Mafanikio:Ban

Mkutano wa Rio+20 Ulikuwa na Mafanikio:Ban

 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema mkutano wa maendeleo endelevu wa Rio+20 uliomalizika wiki jana ulikwa wa mafanikio. Akizungumza Alhamisi kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu matokeo ya mkutano huo Ban amesema kwenye mkutano huo wameshuhudia zaidi jinsi mabadiliko yanavyohitajika na kuongeza kuwa umetoa msingi wa ujenzi wa mustakhbali endelevu.

Ban amesema kuna mambo mengi mazuri yaliyojitokeza katika mustakhbali ambao dunia inautaka, mambo hayo ni pamoja na ari ya kuhakikisha juhudi za kuleta maendeleo endelevu, pili nchi wanachama wameafikiana kuanzisha mchakato wa kimataifa wa maendeleo endelevu kwa wote SDG’s ambao utakwenda sambaba utekelezaji wa maelengo ya maendeleo ya milenia na pia kuendelea baada ya mwaka 2015 ambao ni muda wa kutimiza malengo hayo.

Hivyo Ban amesema ni mwanzo mzuri wa kuhakikisha kila mtu anatekeleza jukumu lake kuleta mustakhbali unaohitajika duniani.