Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO na OIE wazindua Mchakato kudhibiti Ugonjwa wa Shuna

FAO na OIE wazindua Mchakato kudhibiti Ugonjwa wa Shuna

Shirika la chakula na kilimo, FAO pamoja na shirika la kimataifa la afya ya wanyama, (OIE), yamezindua kwa pamoja mchakato wa kimataifa, wa kukabiliana na ugonjwa wa shuna, unaoathiri midomo na miguu ya mifugo.

Mashirika hayo mawili yamesema dhamira na hatma ya mchakato huo ni kutokomeza kabisa ugonjwa huo duniani. Hata hivyo, mashirika hayo yamesema kuwa yataweza kufikia hilo tu ikiwa wadau wengine kote duniani watajitolea na kuunga mkono juhudi hizo kwa ari moja.

Shirika la FAO linasisitiza kuwa ushirikiano na ari ya pamoja itaweza kusaidia kuudhibiti ugonjwa huo, ambao ni mzigo mkubwa kwa mamilioni ya wakulima, wafugaji wa kuhamahama na wafanyibiashara katika bidhaa za kilimo na ufugaji. Jason Nyakundi anaripoti.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)