Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi kuchagiza Afya ya Uzazi na Vita dhidi ya HIV Afrika Mashariki

Viongozi kuchagiza Afya ya Uzazi na Vita dhidi ya HIV Afrika Mashariki

Kufuatia kuzinduliwa kwa mchakato wa kuzuia maambukizi ya virusi vya HIV na afya ya uzazi kwa vijana wa Afrika ya Mashariki na Kusini mwa Afrika mwaka 2011, serikali ya Ujerumani, Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu UKIMWI, UNAIDS na Shirika la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO, yameweka kamati ya viongozi wa kisera na wataalam ambao watuongoza mchakato huo

Kamati hiyo itajumuisha Dr. Sheila Tlou, ambaye ni Mkurugenzi wa timu ya wasaidizi wa UNAIDS katika kanda ya Afrika ya Masahariki na kusini, mkewe rais wa Tanzania, Bi Salma Kikwete na rais wa Zamani wa Botswana Festus Mogae na viongozi wengine 10 kutoka Nyanja za elimu, afya na maendeleo kutoka kanda nzima. George Njogopa na taarifa kamili.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)