Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya wakimbizi wa Syria nchini Iraq yapanda hadi 5,839:UNHCR

Idadi ya wakimbizi wa Syria nchini Iraq yapanda hadi 5,839:UNHCR

Takriban jamaa 25 na watu 200 binafsi wanaendelea kuingia kwenye jimbo la Kikurdi la Iraq na kujiandikisha na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR, na idara ya uhamiaji ya jimbo hilo kila wiki, limesema shirika la UNHCR.

Kuongezeka kwa idadi ya watu wanaowasili upya ikilinganishwa na wiki iliyopita, kumeshuhudiwa katika kipindi cha kutoa ripoti mpya ya UNHCR. Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanapanua juhudi za kuboresha hali ya maisha katika kambi ya Domiz, na kuchunguza hali ya wakimbizi wageni. Uchunguzi kama huo umepangwa kufanyiwa wakimbizi wote wapya kwenye jimbo zima la Kikurdi kati ya Julai 1 na 10.

Idara ya uhamiaji ya serikali ya jimbo hilo inaendelea kuwahoji watu binafsi wanaowasili. Wengi wa wale waliohojiwa kufikia sasa ni raia ambao wanafuta usalama wa kimataifa. Mpakani, visa vya kukamatwa na kuzuiliwa wakimbizi vimeripotiwa kwenye maeneo ya Mosul na Rabiaa. UNHCR inaendelea na juhudi zake za kuwalinda wakimbizi hawa na kuwawakilisha kwenye vitu vya polisi na kotini.