Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yatoa mafunzo ya usalama wa taifa kwa maafisa wa Nigeria

IOM yatoa mafunzo ya usalama wa taifa kwa maafisa wa Nigeria

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM limeanza kuwapatia mafunzo ya usalama wa taifa maafisa uhamiaji wa Nigeria ili kukabiliana na sokomoko lolote kwenye eneo hilo.

Mafunzo hayo ambayo yanatolewa kwa ushirikiano na serikali ya Nigeria yatahitimika kwa kuanzisha kitengo maalumu cha Inteligensia mjini Abuja.

Jumla ya washiriki 21 wamehudhuria mafunzo hayo yaliyogharimiwa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya iliyotenga kiasi cha dola za kimarekani milioni 12.7. Nigeria kwa sasa inaona kuwepo kwa umuhimu mkubwa wa kuongeza uwezo wa kiitelijensia kwa wataalamu wake hasa wakati huu kunakoshuhudia wimbi la matukio yasiyotarajiwa.