Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MONUSCO yatoa mafunzo kwa polisi wa DR Congo

MONUSCO yatoa mafunzo kwa polisi wa DR Congo

Vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo vinasaidia kuwapa mafunzo polisi ili kulinda vituo vya kibiashara kwenye mkoa ulio na utajiri wa madini wa Kivu ulio mashariki mwa nchi.

Uhaba wa maafisa wa usalama waliopewa mafunzo umesababisha serikali ya DRC kupoteza fedha nyingi. Kuna matumaini kuwa mafunzo hayo yatasaidia kutatua mizozo katika eneo la maziwa makuu kwa ujumla na hususan mashariki mwa DRC. Maafisa hao walipewa mafunzo kuhusu jukumu watakalotekeleza kama maafisa wa polisi kwenye migodi nchini humo.

Mafunzo hayo yalilenga usalama wa kibinafsi, haki za binadamu na uporaji wa raslimali. Mafunzo hayo yanafadhiliwa na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM ambapo kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda amani nchini DRC MONUSCO kilipewa jukumu la kusaidia serikali kupambana na uporaji wa raslimali zake.