Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waomba ufadhili ili kuwalinda raia Mashariki mwa Chad

UM waomba ufadhili ili kuwalinda raia Mashariki mwa Chad

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limetoa wito kwa wanachama wake kuhakiisha kuwa kuna ufadhili wa kutosha kwa kikosi cha Chad kilicho na jukumu la kuwapa usalama takriban wakimbizi 600,000 wakati Umoja wa Mataifa utakapoondoka eneo hilo ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

Kikosi cha Umoja wa Mataifa kujulikanacho kama MINURCAT kilichobuniwa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa mwaka 2007 kulinda raia nchini Chad na Jamhuri ya Afrika ya kati na pia kutoa misaada kwa maelfu ya watu waliokimbia mizozo katika nchi hizo mbili kinaondoka kufuatia ombi la serikali ya Chad ikisema kuwa ina jukumu la kuwapa ulinzi raia walio katika ardhi yake.

Umoja wa Mataifa umekaribisha ahadi iliyotolewa na Chad pamoja na kazi inayofanywa na shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP na shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR na mipango inayofanywa na UNDP kuwasaidia wakimbizi hao.