Ofisi ya haki za binadamu yatoa ripoti kuimarisha mfumo wa mikataba

22 Juni 2012

Kamishina Mkuu wa haki za binadamu leo ametoa ripoti ya kurasa 100 akiyataka mataifa kuchukua hatua zitakazoimarisha chombo cha mfumo wa mikataba cha Umoja wa Mataifa ambacho kimekuwa katika shinikizo kwa miaka ya karibuni.

Ripoti hiyo ambayo imekuwa ikiandaliwa kwa miaka mitatu inasema ongezeko la mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu na ongezeko la nchi ambazo zinaridhia mikatab hiyo haiendi sambamba na ongezeko la fedha linaloruhusu kamati za kufuatilia utekelezaji wa mikataba hiyo kufanbyakazi inavyotakiwa.

Kamishna Mkuu amesema katika ripoti hiyo kwamba kimsingi kila kipengee cha mfumo wa mkata kimeongezeka mara mbili tangu mwaka 2000. Ripoti inabainisha matatizo yanayokamili mfumo uliopo ns kusema hsli ys sasa haistahili kuendelea.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter