Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu ya wakimbizi wa Sudan wanahitaji msaada wa dharura-UNHCR

Maelfu ya wakimbizi wa Sudan wanahitaji msaada wa dharura-UNHCR

Hali mbaya ya kibinadamu inaanza kujitokeza miongoni mwa maelfu ya wakimbizi wa Sudan ambao wamekimbilia usalama Sudan Kusini na Ethiopia, kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR. Takriban wakimbizi 200,000 wa Sudan ambao wametoroka mapigano kwenye jimbo la Blue Nile, hivi sasa wamepewa makazi katika kambi za wakimbizi Sudan Kusini na Ethiopia.

Shirika la UNHCR linasema, hali ya kibinadamu inaendelea kuzorota katika kambi hizo kila uchao, huku idadi kubwa ya watoto wakikumbwa na utapia mlo. Shirika hilo la wakimbizi linatoa wito kwa wafadhili kusaidia juhudi za kutoa msaada wa kibinadamu, ambao gharama yake sasa inakadiriwa kuwa takriban dola milioni 219.

Msemaji wa UNHCR, Adrian Edwards anasema, dola milioni 45 za msaada walizopokea kufikia sasa, zimekwisha.