Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ghasia za kidini nchini Nigeria huenda zikawa uhalifu dhidi ya ubindamu:OHCHR

Ghasia za kidini nchini Nigeria huenda zikawa uhalifu dhidi ya ubindamu:OHCHR

 

Ofisi ya haki za binadamku ya Umoja wa Mataifa OHCHR inasema kuwa idadi ya watu waliouawa kutoakana na ghasia za hivi majuzi zinazoendeshwa na kundi la Boko Haram kwenye makanisa nchini Nigeria imeongezeka hadi zaidi ya watu 100.

Kamishina mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa anaonya kuwa vitendo kama hivyo vinavyohusiana na uhasama wa kidini au kujamii huenda vikageuka na kuwa uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Amewataka viongozi wa kikristo na kiislamu nchini Nigeria kufanya jitihada za kuzuua kile mabacho amekitaja kuwa kutowepo uvumilivu kati ya dini. Rupert Colville ni masemaji ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa.