Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa Rio+20 wahitaji uongozi jasiri na wa kujitolea

Mkutano wa Rio+20 wahitaji uongozi jasiri na wa kujitolea

Tume ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya kiuchumi na kijamii kwa maeneo ya Asia na Pasifiki (ESCAP), imesema muda haupo tena wa kupoteza, na kwamba masuala muhimu ni lazima yazingatiwe na mkutano wa Rio+20, ili kupunguza hali inayochangia uharibifu wa mazingira na kuongeza mabadiliko ya hali ya hewa.

Tume hiyo imeyataja masuala hayo kama umaskini, njaa, ukoseu wa ajira, na kuendelea kupungua kwa mali ya asili.

Katibu Mkuu wa tume ya ESCAP, Dr. Noeleen Heyzer, amesema mkutano wa Rio ni fursa ya kipekee katika kizazi kizima ya kubadili mitazamo kuwa vitendo vya kijasiri. George Njogopa anaripoti

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)