Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Masoko matano ya hisa yajitolea kuimarisha uwekezaji endelevu

Masoko matano ya hisa yajitolea kuimarisha uwekezaji endelevu

Mkurugenzi wa Shirika la bishara na maendeleo la Umoja wa Mataifa UNCTAD Supachai Panitchpakdi ametangaza mpango mpya wa masoko ya hisa wa kuwa na uwekezaji wa muda mrefu kwa masoko yao.

Makubaliano hayo ni kati ya soko la hisa la Marekani NASDAQ na na masoko ya hisa kwenye mataifa ya Brazil, Misri, Istanbul na Afrika Kusini.

Kwa ujumla masoko hayo yana zaidi ya makambuni 4600 yaliyosajiliwa. Supachai amesema kuwa ni vyema kuyatambua masoko ya hisa yaliyochukua hatua hizo na kuyataka mataifa zaidi kuchukua mkondo kama huo. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)