Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Naibu Mkuu wa Kaki za Binadamu aanza ziara Malawi

Naibu Mkuu wa Kaki za Binadamu aanza ziara Malawi

 

Naibu Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Kyung-wha Kang, ameanza ziara ya siku nne nchini Malawi ili kujadili masuala kadha wa kadha ya haki za binadamu na rais Joyce Banda na wadau wengine nchini humo.

Hii ndiyo ziara ya kwanza ya aina yake nhcini humo, ya afisa mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa. Mbali na kukutana na rais Banda, Bi Kang atafanya mazungumzo na baadhi ya maafisa wakuu wa serikali, wakiwemo mawaziri, uongozi wa bunge, tume ya haki za binadamu ya Malawi, mashirika ya umma na mashirika ya Umoja wa Mataifa.

 Kabla ya safari yake, Bi Kang amesema huu ni wakati muhimu wa mabadiliko makubwa kwa Malawi, na kwamba afisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inatarajia kushirikiana na serikali na mashirika ya umma, katika kusaidia kuendeleza na kuhakikisha haki za binadamu kwa wote.