Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Eritrea yashtumiwa kwa ukiukaji mkubwa wa haki za Binadamu

Eritrea yashtumiwa kwa ukiukaji mkubwa wa haki za Binadamu

Takriban wafungwa 10,000 wa kisiasa wapo katika jela nchini Eritrea, kwa mujibu wa Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, Navi Pillay.

Katika hotuba yake kwa Baraza la Haki za Binadamu, Bi Pillay amesema kuwa hatma ya wafungwa hawa haijulikani, kwani Eritrea imekataa kushirikiana na afisi yake na mifumo mingine ya haki za binadamu ya kimataifa nay a kikanda.

Kamishna huyo mkuu amesema duru za kuaminika zimeweka daftari za ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, ukiwemo kuwafunga watu kinyume na sheria, utesaji, mauaji ya kikatili, kuwashinikiza kufanya kazi, na kuingizwa katika jeshi, pamoja na kutokuwepo uhuru wa kusafiri, kujieleza, kufanya ibada, na mikutano.

Bi Pillay pia ameelezea kusikitishwa kwake na kuzorota kwa hali ya haki za binadamu nchini Mali, baada ya mapinduzi ya kijeshi.

(SAUTI YA NAVI PILLAY)