Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wajadili visiwa vya Falklands(MALVINAS)

UM wajadili visiwa vya Falklands(MALVINAS)

Kamati maalum kuhusu kuondoa ukoloni imesema kuwa kuondoa hasa hali maalum ya ukoloni inayohusiana na visiwa Falklands au Malvinas, kunahitaji muafaka kwa njia ya amani baina ya Argentina na Uingereza kuhusu uhuru wa visiwa hivyo.

Kwa azimio la pamoja lililopendekezwa na Waziri msaidizi wa Mambo ya nje wa Chile, kamati hiyo maalum imesikitika kuwa, licha ya jamii ya kimataifa kuunga mkono maafikiano kati ya nchi hizo mbili, utekelezaji wa maazimio ya Baraza Kuu kuhusu suala hili haujaanza.

Serikali za Argentina na Uingereza zimeombwa kuimarisha juhudi zilizopo sasa za mazungumzo na ushirikiano ili kufikia muafaka kwa njia ya amani kuhusu suala la visiwa vya Falklands, chini ya maazimio 2065 (20) na 3160 (28).