Baraza kuu la UM lamteua Vuk Jeremic kuwa rais wa kikao cha 67 cha baraza hilo

11 Juni 2012

Baraza Kuu la Umoja wa Mataiafa limemteua waziri wa mambo ya kigeni wa Serbia Vuk Jeremic kuwa raia wa kikao kinachokuja cha 67 cha bazara kuu la Umoja huo.

Kwenye shughuli ya kupiga kura ya kuchagua rais mapema leo bwana Jeremic alipata kura 99 ambapo mpinzani wake balozi Dalius Cekuolis kutoka Lithuania alipata kura 85.

Bwana Jeremic alitoa shukran nyingi kwa kuchaguliwa kwake akiongeza kuwa lengo kuu la kikao cha 67 litakuwa ni kuangazia utatuzi wa mizozo ya kimataiafa kwa njia ya amani. Baraza kuu la Umoja wa Mataifa lenye wanachama 193 huwa linatoa nafasi ya kujadili kwa kina masusla ya kimataifa na huwa linakutana kila mwaka kati ya mwezi Septemba na Disemba.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter