Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya wafanyakazi katika eneo linalokaliwa la Palestina bado ni mbaya:ILO

Hali ya wafanyakazi katika eneo linalokaliwa la Palestina bado ni mbaya:ILO

Hali ya wafanyakazi katika maeneo ya Waarabu yanayokaliwa inatia uwoga na bado ni mbaya, kwa mujibu wa ripoti ya mwaka ya shirika la kazi duniani ILO, iliyowasilishwa kwenye mkutano wa shirika hilo mjini Geneva.

Ripoti inasema hali hii imesababishwa na ukweli wa kukaliwa kwa maeneo hayo na upanzi wa makazi ya walowezi wa Kiyahudi unaofanywa na Israel, na hivyo kusababisha fursa ya Wapalestina ya kuendelea kuzidi kuwa finyu.

Ripoti inasema hali halisi inadhihirika katika area C kwenye Ukingo wa Magharibi eneo ambalo ni muhimu kwa mustakhbali wa taifa la Wapalestina. Eneo hilo lina asilimia 60 ya Wapalestina lakini linaendelea kuwa chini ya udhibiti wa Israel.

Mkrugenzi wa ILO Juan Soamavia anasema mchakato wa amani bado uko njia panda, na hali iliyoko katika maeneo yanayokaliwa inapunguza matumaini ya majadiliano baina ya suluhu ya kuwa na mataifa mawili.

(SAUTI YA KARI TAPIOLA)