Balozi Mahiga atoa wito Msaada Uongezwe Kuisaidia Somalia

31 Mei 2012

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa katika maswala ya Somalia, Augustine Mahiga, ametowa wito kwa jamii ya kimataifa iongeze juhudi zake katika kulisaidia taifa hilo la pembeni mwa Afrika. Mahiga amesema haya wakati wa mkutano wa pili wa kimataifa kuihusu Somalia.

Mkutano huo wa siku mbili ujulikanao kama Istanbul 2, unakutanisha sekta ya kibinafsi, wafadhili, serikali ya Somalia, Umoja wa Mataifa na mashirika ya umma, na unaangazia wajibu na majukumu ya jamii ya kimataifa katika kusaidia kuikwamua Somalia na kusaidia kuiendeleza, pamoja na mabadiliko ya kisiasa yanayoendelea sasa.

Baada ya miongo ya migogoro, Somalia imekuwa kwenye juhudi za amani na maridhiano, huku serikali yake ya mpito ikiwa inatekeleza mpango ulobuniwa mwezi Septemba mwaka jana, ambao unaweka vitu vinavyostahili kupewa kipaumbele kabla ya kipindi cha serikali ya mpito kukamilika Agosti 20

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter