Skip to main content

Kamati ya UM yalaani Mauaji ya Watoto Syria

Kamati ya UM yalaani Mauaji ya Watoto Syria

Kamati ya Umoja wa Mataifa ya haki za mtoto imelaani vikali mauaji ya watu 108 wakiwemo watoto 49 huko El Houleh Syria Ijumaa na Jumamosi iliyopita.

Kamati hiyo ambayo inakutana Geneva inasema pia inatiwa hofu na ripoti kutoka kwa waangalizi wa Umoja wa Mataifa za kuendelea kwa ghasia na mauaji ya raia.

Kwa mujibu wa kamati hiyo watoto wengi waliouawa Syria ni wa chini ya umri wa miaka 10. Katika taarifa yao iliyotolewa leo inazidi kutiwa hofu kutokana na ukweli kwamba tangu kuanza kwa maandamano Syria Machi mwaka jana mamia ya watoto wameawa, kujeruuhiwa na kuwekwa rmande. Licha ya wito ambao mekuwa ukitolewa kwa serikali na pande zingine husika kusitisha ghasia, wito huo haujasaidia na hakuna hatua zilizochukuliwa.

Kamati imeitaka serikali ya Syria kuhakikisha kwamba wahusika wa mauaji ya El Houleh na wale wote walioshiriki uhalifu ho dhidi ya watoto wawajibishwe.