Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu Milioni 2 Huenda Wakakumbwa na Ukame Angola:OCHA

Watu Milioni 2 Huenda Wakakumbwa na Ukame Angola:OCHA

Hadi watu milioni 2 huenda wakakumbwa na ukame nchini Angola, kwa mujibu wa ripoti ambayo imetolewa na Idara ya kuratibu huduma za msaada wa kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, OCHA na wadau wengine. Ripoti hiyo ambayo imetolewa na afisi ya eneo la Kusini mwa Afrika, inaangazia kipindi cha Aprili 01 hadi Mei 24 mwaka 2012.

Idadi karibu sawa na hii imetajwa pia na wizara ya kilimo na ufugaji ya serikali ya Angola, ambayo inawakilisha jamii zaidi ya laki tatu.

Angola ilipokea chini ya asilimia 60 pekee ya mvua ya msimu wa kawaida wa mvua, ambao huwepo kutokea Septemba hadi mwanzoni mwa Mei, ambayo ilichangia kupungua kwa uzalishaji wa chakula kote nchini kwa tani 400, 000. Jason Nyakundi anaripoti.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)