Skip to main content

Kiongozi wa Sierra Leone ahaidi Uchaguzi Huru

Kiongozi wa Sierra Leone ahaidi Uchaguzi Huru

Licha ya changamoto zinazoikabili Sierra Leone, nchi hiyo imepiga hatua kubwa tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe miaka 10 iliyopita kwa mujibu wa mwakilishi wa Afrika ya Kusini kwenye Umoja wa Mataifa.

Balozi Baso Sangqu ameyasema hayo wakati baraza la usalama linasikiliza taarifa kuhusu mpango wa Umoja wa Mataifa Afrika ya Magharibi kwa nchi za Liberia, Ivory Coast na Sierra Leone. Balozi Sangqu alikwa kiongozi mwenza wakati ujumbe wa wanachama 15 wa baraza la usalama ulipozuru Sierra Leon.

Balozi huyo amesema uchaguzi wa Rais na wabunge uliopangwa kufanyika Novemba mwaka huu ulijadiliwa wakati ujmbe wa baraza ulipokwa nchini humo.

Amesema Rais Koroma wa Sierra Leone alihakikishia ujumbe huo kuwa kutakuwa na chaguzi huru, wa haki na wa uwazi. Na mazungumzo na vyama vyote vya kisiasa na tume ya uchaguzi waliuhakikishia ujumbe kwamba hatua zimepigwa katika kuandaa uchaguzi huo wa Novemba.