Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UNHCR anasema kuna Ongezeko la Migogoro

Mkuu wa UNHCR anasema kuna Ongezeko la Migogoro

Inakuwa ni vigumu kupata suluhu kwa watu walioko katika hali ya ukimbizi duniani amesema mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhdumia wakimbizi UNHCR.

Antonio Guterres katika uzinduzi wa ripoti ya hali ya wakimbizi duniani Alhamisi amesema sio kitabu kuhusu takwimu bali ni uchambuzi wa tatizo la wakimbizi na changamoto za kuwasaidia wakimbizi hao.

Bwana Guterres amesema migogoro mipya iliongezeka mwaka jana na kusababisha wimbi kubwa la wakimbizi wapya katika muongo uliopita. Bwana Guterres ametaja migogoro mitatu aliyosema ni mibaya sana ambayo ni Syria, Sudan Kusini na Sudan, pia Mali, ukiacha mbali watu waliokuwa wakikimbia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuingia Uganda na Rwanda.

Amesema wakati migogoro mipya ikizuka ya zamani haitoweki, kwani Afghanistan bado upo, Somalia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo vilevile. Na hivyo asilimia 70 ya wakimbizi wote duniani waliochini ya NHCR pamoja na wakimbizi wote wa Palestina leo hii bado wako katika hali ya ukimbizi, ikimaanisha kwamba wamekwa wakimbizi kwa zaidi ya miaka mitano na inazidi kwa vigumu kupata suluhisho lao.