Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani

Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ametoa ujumbe maalum wa pongezi kwa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa, wakati wa kuadhimisha siku ya kimataifa ya walinda amani.

Wakati akiweka ua la heshima kwa ajili ya wanajeshi 112 waliofariki dunia mnamo mwaka 2011, Bwana Ban amewashukuru wanajeshi 120, 000 walinda amani wa Umoja wa Mataifa, na kuongeza kuwa, daima anafurahia na kujivunia juhudi za wanawake na wanaume wanaojitahidi kwa ajili ya kulinda amani. Amesema, lengo la Umoja wa Mataifa katika kulinda amani, ni kuhakikisha kuimarishwa kwa usalama na utulivu katika maeneo yenye mizozo ili kusiwe tena na haja ya kuwa na vikosi vya kulida usalama.

Hervé Ladsous ambaye ni Mkuu wa Shughuli za Kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa, ameelezea ujasiri wa vikosi hivi.

(SAUTI YA HARVE LADSOUS)

Captain Rachel Kagia, ni afisa katika kikosi cha Walinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Congo MONUSCO.

(SAUTI YA RACHEL KAGIA