Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNDP yazindua ripoti inayoangazia Usalama wa Chakula barani Afrika

UNDP yazindua ripoti inayoangazia Usalama wa Chakula barani Afrika

Shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP leo limezindua ripoti ya maendeleo kwa afrika na kutaja tatizo la njaa ni msamiati uliokosa ufumbuzi wa muda mrefu na hivyo imehimiza mapinduzi ya fikra ili kukwamua janga hilo. Ripoti hiyo ambayo imebeba dhima isemayo kuelekea kwenye mustakabala wenye uhakika wa chakula, imeeleza kuwa ongezeko endelevu kwenye uzalishaji chakula na lishe bora ndiyo vichocheo vya ukuaji katika kujitosheleza kwa chakula na maendeleo ya binadamu.

Kutoka dsm, ambako ndiko kulikozinduliwa ripoti hiyo George Njogopa anaarifu zaidi.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)