Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utokomezaji wa Polio unasuasua kutokana na Ukosefu wa Fedha:WHO

Utokomezaji wa Polio unasuasua kutokana na Ukosefu wa Fedha:WHO

Juhudi za kutokomeza polio duniani zinaweza kusita katika miaka miwili ijayo endapo dola bilioni moja zilizopungua kufadhili juhudi hizo hazitopatikana limesema shirika la afya duniani WHO.

Fedha zinahitajika ili kuongeza kampeni za chanjo nchini Nigeria, Pakistan na Afghanistan maeneo ambayo yamesalia na matatizo ya polio. WHO inasema mpango wa kkimataifa wa kutokomeza polio unapungza kampeni zake katika nchi 24 ambazio zilimekuwa katika hatari ya maambukizi ya virusi vya maradhi hayo ili kufadhili kampeni Nigeria, Pakistan na Afghanistan. Visa 55 vya polio vimeripotiwa mwaka huu. Dr Bruce Aylward ni mkuu wa idara ya polio kwenye shirika la WHO.

(SAUTI YA DR BRUCE AYLWARD)

Shirika la WHO linakadiria kwamba watoto milioni mbili huenda wakapooza endapo polio haitotokomezwa katika muongo ujao.