Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yataka mkazo zaidi Kupunguza Vifo vya Watoto

UNICEF yataka mkazo zaidi Kupunguza Vifo vya Watoto

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na watoto UNICEF limetoa mwito likitaka kuchukuliwa kwa hatua madhubuti kudhibiti tatizo la kuzama majini, tatizo ambalo utafiti wa hivi karibuni umebainisha kuwa ni miongoni mwa yanayosababisha vifo vingi katika eneo la Asia.

Hali ya kuzama maji inatajwa kuwa ndiyo inayoongoza kwa kusababisha vifo vya watoto wengi walio kati ya umri wa mwaka 1 hadi 17. Matatizo hayo yapo katika alama ya juu katika nchi za Bangladesh, Cambodia, Thailand, Viet Nam na majimbo ya Beijing na Jiangxi ya nchini China.

Tafiti zinasema kuwa kwenye nchi hizo pekee kila watoto wanne wanaofariki basi moja ni kutokana na tatizo hilo, kiwango ambacho ni kikubwa zaidi ukilinganishwa na matatizo mengine kama polia, tetanus, surua.