Skip to main content

Mkutano wa Rio+20 ni fursa nzuri wa dunia:Ban

Mkutano wa Rio+20 ni fursa nzuri wa dunia:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameyataka mataifa kutumia fursa inayokuja ya mkutano kuhusu maendeleo endelevu wa Rio+20 ili kuiweka dunia kwenye mkondo kuelekea nyakati zenye matumaini akiongeza kuwa ushirikiano litakuwa jambo muhimu katika kupata suluhu la changamoto zinazoukumba ulimwengu.

Ban amesema kuwa mkutano wa Rio utakuwa fursa nzuri katika kuangazia masuala ya uchumi , ya jamii, na mazingira. Zaidi ya marais 30 wakiwemo maelfu ya wabunge, mameya, maafisa kutoka Umoja wa Mataifa na viongozi wa mashirika ya kijamii watakutana kwenye mkutano wa Rio+20 mjini Rio de Janeiro nchini Brazil mwezi ujao wa Juni kuweka sera na hatua zenye lengo la kupunguza umaskini na kulinda mazingira.