Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Fedha zahitajika sasa kulisaidia eneo la Sahel:Raul Gonzalez

Fedha zahitajika sasa kulisaidia eneo la Sahel:Raul Gonzalez

Mwana kandanda wa Uhispania, Raul Gonzalez ambaye ni balozi mwema wa FAO ametoa wito kwa jamii ya kimataifa itoe msaada wa dharura kwa eneo la Sahel Afrika Magharibi ili kuzuia majanga ya utapia mlo na ukosefu wa lishe bora.

Raul amesema hayo wakati akilizuru taifa la Chad ambalo linakabiliwa na ukame. Takriban watu milioni 17 wanakabiliwa na janga la njaa, na zaidi ya watoto milioni moja chini ya umri wa miaka mitano wanakabiliwa na utapia mlo. Ukame, umaskini, mfumko wa bei ya chakula pamoja na watu kukimbia makwao kwa ajili ya migogoro kumesababisha kushuka kwa uzalishaji wa chakula katika eneo zima la Sahel. Jason Nyakundi na ripoti kamili.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)