Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano kuhusu Kuondoa Silaha za Nyuklia Waidhinisha Ratiba ya Masuala Muhimu

Mkutano kuhusu Kuondoa Silaha za Nyuklia Waidhinisha Ratiba ya Masuala Muhimu

Mkutano wa kimataifa kuhusu uondoaji wa silaha, umeidhinisha leo ratiba ya matukio muhimu na kufanya mazungumzo kuhusu kukomesha mzozo na silaha za nyuklia, pamoja na kuzuia vita vya nyuklia.

Mwenyekiti wa mkutano huo anayeondoka, Balozi Minelik Alemu Getahun wa Ethiopia, amesema kuwa muhimu hasa kwa mwenyekiti yeyote wa mkutano huo, itakuwa ni kufanya juhudi zozote zile, kuhakikisha kwamba kuna mpango mathubuti wa kufikia malengo hayo. Mnamo siku ya Alhamis, mkutano huo utazingatia jinsi ya kuzuia kuzalisha vitu vinavyotumiwa kutengeza silaha za nyuklia