Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Machafuko nchini Lebanon yatia wasi wasi:Derek

Machafuko nchini Lebanon yatia wasi wasi:Derek

Mratibu Maalum wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya Lebanon, Derek Plumbly, amesema leo kuwa amesikitishwa na matukio ya ghasia hivi karibuni, ambazo zimesababisha vifo Lebanon, pamoja na Tripoli wiki ilopita. Baadhi ya wale walouawa katika machafuko hayo ni Sheikh Ahmad Abdel-Wahid na Sheikh Mohammad Hussein Merhed, na watu wengine mjini Beirut, Lebanon.

Bwana Plumbly amesema ni muhimu kusitokee tena machafuko kama haya, na kufanywe uchunguzi wa kina kuhusu yale ambayo yametokea. Ameongeza kuwa tangu alipowasili Lebanon, amefurahishwa na juhudi zinazofanywa na viongozi wa mambo ya usalama na wale wa kisiasa ili kulinda amani na utulivu, wakati wa migogoro na hali ya sintofahamu katika eneo zima.

Amewahimiza wote nchini Lebanon wazingatie zaidi taifa lao kuliko kitu kingine kile, na kumaliza mizozo kupitia mazungumzo, bila kurejelea ghasia.