Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la 65 la afya laanza mjini Geneva:WHO

Baraza la 65 la afya laanza mjini Geneva:WHO

Kikao cha 65 cha baraza la afya duniani kimeanza Jumatatu mjini Geneva. Katika siku sita zijazo wajumbe kutoka nchi 194 wanachama wanajadili masuala kadhaa ya afya ya jamii ikiwemo, mipango, bajeti, udhibiti na uongozi kwenye shirika la afya duniani WHO.

Pia uteuzi wa Dr Margaret Chan kuwa mkurugenzi mkuu wa WHO kwa muhula wa pili utawasilishwa ili kuidhinishwa. Akizungumza katika ufunguzi wa baraza hilo Bi Chan amesema kazi za uongozi wa WHO mara nyingi zinazaa matunda ingawa ni madogo lakini yenye uwekezaji mzuri. Amesema mfano chanjo ya uti wa mgongo barani Afrika ilizinduliwa kwenye mradi wa WHO na PATH inaleta matumaini ya kumaliza ugonjwa huo Afrika.

Amesema hatua hiyo italeta afueni kubwa kwani gharama za matibabu na kampeni ya chanjo ya uti wa mgongo hugharimu serikali karibu asilimia 5 ya bajeti yote ya afya.

(SAUTI YA MARGARET CHAN)