Sijahusika na Uhalifu wa vita Sierra Leone:Charles Taylor

16 Mei 2012

Rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor ameiambia mahakama maalumu ya Sierra Leone mjini The Hague kwamba hausiki na uhalifu wa vita uliotekelezwa nchini Sierra Leone.

Jumatano mahakama hiyo maalumu imesikiliza uwasilishwaji wa hukumu kutoka upande wa mashitaka, upande wa utetezi na kumsikia bwana Taylor akijitetea.

Taylor amesema yeye sio tishio kwa jamii, na kwamba anaanza mchakato wa kutibu majeraha ya machungu ya vita kwa tume ya kutoa kipaumbele kwa amani na maridhiano kama ile iliyoundwa Afrika ya Kusini.

Taylor ameongeza kuwa anazungumza kwa ujasiri kuhusu maridhiano na sio adhabu, na ametaka huo uwe muongozo katika jukumu la mahakama hiyo.

(SAUTI YA CHARLES TAYLOR)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter