Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Raia wa Afghanistan wahitaji msaada wa dharura, asema Valerie Amos akikamilisha ziara yake ya kwanza nchini humo

Raia wa Afghanistan wahitaji msaada wa dharura, asema Valerie Amos akikamilisha ziara yake ya kwanza nchini humo

Mratibu Mkuu wa Maswala ya Dharura katika Umoja wa Mataifa, Valerie Amos, amesema kuwa raia wa Afghanistan wanahitaji msaada wa dharura, na ambao wanastahili kufikishiwa bila upendeleo. Bi Amos amesema haya mwishoni mwa ziara yake ya kwanza nchini Afghanistan, ambako amekuwa akikagua mahitaji ya kibinadamu.

Ameongeza kusema kuwa, jamii ya kimataifa itaendelea kutoa msaada wa kibinadamu pale ambapo unahitajika, lakini ni dhahiri kuwa, hii pekee haitoshi. Pia, amesema ni sharti zitiliwe mkazo juhudi za kuhakikisha uwezo wa jamii kujikimu zenyewe, pamoja na kuongeza nguvu na uwezo wa tasisi za kutoa huduma muhimu. Bi Amos amesema kumekuwa na ufanisi mkubwa katika mwongo mmoja ulopita, ingawa bado Afghanistan ipo chini kabisa ya daraja la maendeleo ya kibinadamu, na hivyo basi, bado kuna kazi nyingi ya kufanya.