Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa FAO aonya kuhusu upungufu wa fedha kusaidia pembe ya Afrika na Sahel

Mkuu wa FAO aonya kuhusu upungufu wa fedha kusaidia pembe ya Afrika na Sahel

Mkurugenzi mkuu wa shirika la chakula na kilimo FAO Jose Graziano da Silva Alhamisi ameonya kwamba kuna upungufu mkubwa wa fedha za kufadhili shughuli zilizopangwa na FAO kwenye maeneo ya Sahel na Pembe ya Afrika.

Akizungumza kwenye kongamano la kimataifa mjini Madrid da Silva amesema ingawa kuna maelewano ya jinsi ya kuongeza usalama wa chakula na maendeleo, hivi sasa kuna tatizo kubwa nalo ni fedha. George Njogopa na maelezo zaidi.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)