Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mafunzo ya Buddha ni muhimu kwa maisha ya baadaye:Ban

Mafunzo ya Buddha ni muhimu kwa maisha ya baadaye:Ban

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa mafunzo wa Buddha yanaweza kutoa mchango katika kuiboresha dunia kwa maisha mema yajayo. Ban amesema kuwa mafunzo hayo yanazipa changamoto jamii na mataifa kufanya hima kukakikisha kuwepo maisha mema. Amesema kuwa mafunzo hayo yana maana hasa wakati huu ambapo nchi zinapojiandaa kwa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo wa Rio nchini Brazil mwezi ujao mkutano ambao Ban ameutaja kuwa fursa nzuri kwenye kizazi hiki katika kuuweka ulimwengu kwenye mkondo wa maendeleo. Ban amewataka watu kutoka tamaduni mbali mbali kutumia siku ya Vesak kungazia jinsi wanavyoweza kuboresha maisha yao ya baadaye.