Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akutana na kiongozi wa upinzani nchini Myanmar

Ban akutana na kiongozi wa upinzani nchini Myanmar

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekutana na kiongozi wa upinzani nchini Myanmar Aung San Suu Kyi kwa mara ya kwanza akiwa ziarani nchini humo. Ban amesema kuwa Suu Kyi amekubali mwaliko wa kumuomba autembelee Umoja wa Mataifa mjini New York.

Mkutano kati ya wawili hao ulifanyika nyumbani kwake Suu Kyi eneo la Rangoon siku moja baada ya kula kiapo kama mbunge. Mkutano kati ya wawili hao ulifanyika nyumbani kwake Suu Kyi eneo la Rangoon siku moja baada ya kula kiapo kama mbunge. Akiwa nchini Myanmar Ban ametaka kuendeshwa kwa biasahara kwa njia bora kuamabata na haki za binadamu . Ameongeza kuwa biashara ndiyo nguzo ya ukuaji wa uchumi.