Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya UM yatuma misaada visiwa vya Comoro

Mashirika ya UM yatuma misaada visiwa vya Comoro

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yakiwemo shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA, la kuwahudumia watoto UNICEF na la mpango wa chakula duniani WFP yametuma misaada ya dharura kwenda visiwa vya Comoro ambapo serikali imetangaza hali ya hatari kufuatia mvua nyingi na mafuriko makubwa.

Visiwa hivyo vilivyo kati ya Madagascar na Musumbiji vimekumbwa na kiasi kikubwa cha mvua tangu tarehe 20 mwezi uliopita na kusababisha mafuriko pamoja na maporomoko ya udongo. Kulingana na serikali ya Comoro na mashirika mengine ya kibinadamu karibu watu 50,000 wameathiriwa na mvua hizo huku watu 9,000 wakilazimika kuhama makwao. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)