Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matumizi ya vyakula vya aina tofauti kutaimarisha lishe duniani

Matumizi ya vyakula vya aina tofauti kutaimarisha lishe duniani

Kutilia maanani suala la matumizi ya aina nyingi ya vyakula vya kiasili ni jambo linaloweza kutoa mchango mkubwa kwenye usalama wa chakula na kwenye lishe na kuboresha afya za watu. Hii ni kwa mujibu wa maafisa kwenye uzinduzi wa mradi mpya wa kimataifa kwenye mkutano wa dunia wa lishe wa Rio.

Shirika la kimataifa linatoa ufadhili kwa mkiradi ya kimazingira GEF kwa sasa linafadhili miradi inayoongozwa na mataifa ya Brazil, Kenya , Sri Lanka na Uturuki. Miradi hiyo hiyo inapata usaidizi kutoka kwa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP na lile la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO.