Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Masharti mapya kwa NGO's yanagandamiza haki za binadamu:Pillay

Masharti mapya kwa NGO's yanagandamiza haki za binadamu:Pillay

Kamishina Mkuu wa Haki za Binadam wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay Jumatano ameelezea hofu yake kuhusu hatua ya hivi karibuni katika baadhi ya nchi kuondoa uhuru wa mashirika yasiyo ya kiserikali yaani NGO’s na jumuiya zingine za kiraia kufanya shughuli zao kwa uhuru na inavyostahili.

Mswaada wa sheria kufuatilia NGO’s Misri endapo utapitishwa Bi Pillay amesema utakandamiza ari ya mapinduzi ya jumuiya za kijamii ambazo zimekuwa na jukumu kubwa nchini humo. Amesema sheria hiyo itatoa uwezo mkubwa kwa serikali kufuatilia, kurekebisha na kubana kazi za jumuiya za kijamii. Alice Kariuki anaripoti.

(RIPOTI YA ALICE KARIUKI)