Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wiki ya chanjo yaanza katika nchi 180 duniani:WHO

Wiki ya chanjo yaanza katika nchi 180 duniani:WHO

Kwa mara ya kwanza jumuiya ya waaguzi wa afya katika mabara yote duniani wanajikita kwa wakati mmoja katika umuhimu wa chanjo dhidi ya maradhi yanayoua. Wiki ya chanjo ya shirika la afya duniani WHO imeanza Aprili 21 na itaendelea hadi April 28 mwaka huu katika nchi zaidi ya 180 duniani.

Kauli mbiu ya wiki hii “Linda dunia yako, pata chanjo” ikiwa na lengo la kuchagiza umuhimu wa chanjo na kuwatia shime watu kila mahali kupata chanjo hiyo na watoto wao dhidi ya maradhi ambayo ni ya hatari. Pia ni wakati wa kukumbusha kwamba dunia inazidi kuwa tandawazi na kwamba mlipuuko wa mgonjwa unaweza kuathiri jamii kila mahali. Chanjo ina uwezo wa sio tuu kuokoa maisha bali pia kubadili maisha kwa kuwapa watoto fursa ya kukua wakiwa na afya njema, kwenda shule na kuimarisha matarajio ya maisha yao.