Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bodi ya wakurugenzi wa Benki kuu wamchagua Dr Jim Yong Kim kuwa Rais mpya wa Bank hiyo

Bodi ya wakurugenzi wa Benki kuu wamchagua Dr Jim Yong Kim kuwa Rais mpya wa Bank hiyo

Bodi ya wakurugenzi wa Bank ya dunia wamekutana leo kuchagua rais mpya wa Bank hiyo. Kwa pamoja bodi hiyo imemchagua Dr Jim Yong Kim kuwa Rais mpya wa Bank ya dunia kwa kipindi cha miaka mitano kinachoanza rasmi Julai Mosi mwaka huu 2012.

Dr Kim amechaguliwa baada ya kufuata mchakato mpya wa chaguzi waliokubaliana mwaka 2011 ambao kwa mara ya kwanza katika historia ya Bank hiyo kumekuwa na majina tofauti ya wagombea.

Pia wamemshukuru Rais anayeondoka madarakani Robert B Zoellick kwa uongozi imara na kazi nzuri ya kupunguza umasikini kwa nchi wanachama suala ambalo ni jukumu kubwa la bank hiyo.

Bodi ya wakurugenzi pia imewashukuru wagombea wote akiwemo Jim Yong Kim mwenyewe, Jose Antonio Ocampo na Ngozi Okonjo-Iweala. Ugombea wao umezua mjadala kuhusu jukumu la Rais wa Bank ya dunia na mtazamo wa Bank hiyo katika siku za usoni.

Dr Kim alizaliwa mwaka 1959 nchini Korea Kusini na alihamia Marekani na familia yake akiwa na umri wa miaka mitano.

Amekulia Muscatine Iowa. Alihitimu shahada yake ya kwanza mwaka 1982 kwenye chuo kikuu cha Brown na kisha kupata shahada ya udaktari katika chuo kikuu cha udaktari cha Havard mwaka 1991. Mwaka 1993 alipata PHD kwenye chuo hichohicho cha Havard. Amemuoa Dr Younsook Lim ambaye ana wana watoto wawili wa kiume.