Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Raia wa Timor-Leste wapiga kura katika duru ya pili ya chaguzi wa Rais

Raia wa Timor-Leste wapiga kura katika duru ya pili ya chaguzi wa Rais

Raia wa Timor-Leste Jumatatu wamejitokeza tena kupiga kura ya duru ya pili ya uchaguzi mkuu wa Rais. Watu takriban 600,000 wamejiandikisha kupiga kura wengi wakiwa kutoka mjini mkuu Dili ambapo wapiga kura 120,000 wamejitokeza.

Watu wengi nchini humo upigaji kura wa leo unamaanisha ni kukabiliana na changamoto zilizowaghubika kwa muda mrefu, kwa upande wa mpango wa Umoja wa Mtaifa nchini humo kura ya leo ni mfano mzuri wa utekelezaji wa demokrasia Timor-Leste. Ameerah Haq ni mwakilishi wa Katibuu Mkuu nchini humo.

(SAUTI YA AMEERAH HAQ)