Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WaCongo waliotimuliwa Angola wanapatiwa msaada:OCHA

WaCongo waliotimuliwa Angola wanapatiwa msaada:OCHA

Mashirika ya misaada ya kibinadamu yanawasaidia maelfu ya wahamiaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo waliotimuliwa nchini Angola ambapo wengi wanasema wamefanyiwa vitendo vya ghasia na ukatili.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA limesema mwaka jana Angola iliwafurusha raia wa Congo 100,000 na tangu mwingoni mwa mwaka 2003 Angola imeshawafungisha virago wahamiaji haramu 400,000 wengio wao wakiwa raia kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Waliofukuzwa wengi hawana vibali vya kfanya kaziambao walikuwa wakifanya kazi kwenye migodi ya almasi karibu na mpakani.

Umoja wa Mataifa umetoa dola milioni 2.8 kwa ajili ya Dr Congo fedha zitakazotumiwa na mashirika mbalimbali ya kimataifa na NGO’s kuwasaidia wahamiaji hao waliofukuuzwa. UNICEF na NGO’s zingine zimekuwa zikitoa msaada wa chakla, mavazi, malazi na vifaa vya kupikia kwa watu wanaowasili.