Ban ataka kumalizwa kwa mzozo kati ya Sudan na Sudan kusini

16 Aprili 2012

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amefanya mazungumzo mwishoni mwa wiki na waziri wa mambo ya kigeni nchini Sudan Ali Ahmed Karti ambapo amesistiza umihimu wa kusitishwa kwa mzozo uliopo kati ya Sudan na Sudan kusini akiongeza kuwa njia za kijeshi haziwezi kutatua mzozo uliopo.

Kwenye mahojiano kwa njia ya simu kati ya bwana Karti na Ban wote waliitka serikali ya Sudan kujizuia na kutoa nafasi ya kuwepo mkutano kati ya viongozi wa nchi hizo mbili ili kutatua tofauti zilizopo. Juma lililopita baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lilijadili hali iliyo kati ya mataifa hayo mawili na kuonya kuwa huenda mataifa hayo yakaingia vitani.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter