Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wazisifu nchi zilivyochukua tahadhari kufuatia tishio la tsunami

UM wazisifu nchi zilivyochukua tahadhari kufuatia tishio la tsunami

Umoja wa Mataifa umezipongeza nchi zilizoko kwenye mwambao wa bahari ya hindi namna zilivyochukua tahadhari ya haraka wakati kulipopandishwa kuwepo kwa tishio la kuzuka kwa tsunami kufuatia tetemeko kubwa huko Indonesia.

 Katika taarifa yake, shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na misaada ya usamaria mwema OCHA limesifu uharaka ulionyeshwa na nchi hizo.

 Zaidi ya nchi nane zilizoko kwenye ukanda wa bahari ya hindi, zilipandisha kiwango cha tahadhari huku vikiandaa pia vifaa vya uokoaji.