Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lalaani mashambulizi ya kijeshi nchini Mali

Baraza la Usalama lalaani mashambulizi ya kijeshi nchini Mali

Baraza la Usalama limelaani vikali hatua ya kikundi cha waasi Tuareg kianchoendeleza mashambulizi ya kijeshi katika eneo la Kaskazini mwa Mali.

Waasi hao wanaungwa mkono na kundi la kiislamu lenye msimamo mkali.

Katika taarifa yake, Baraza hilo la Usalama limewataka waasi hao kusitisha hujuma hizo mara moja.

Limewataka pia viongozi wa kisiasa toka pande zote kujongea kwenye meza ya majadiliano kwa shabaha ya kutanzua mikwamo inayojitokeza.